Kuanza na Mungu

Hongera kwa uamuzi wako wa kumwomba Yesu kuingia maishani mwako.

Kutoka hapa twende wapi?

Kama hii ingekuwa dini kiongozi wa dini angekupatia Miongozo aina aina. Sherehe. Matakwa. Na hata pengine wakupatie msururu wa vitu vingi ambavyo unahitaji kununua! Lakini wakati ulimwomba Yesu kuingia maishani mwako hukuingia katika dini, la hasha.

Badala yake wewe ulianza kuwa na uhusiano na Mungu.

Na hilo ni jambo la ajabu sana. Huenda unajiuliza: Je, nawezaje kumjua Mungu vizuri zaidi?

Twakushauri uanze na makala haya mawili:

Tutumie barua pepe. Utapata majibu yako ya kibinafsi kutoka kwa mmoja wetu katika tovuti hii. Tutumie barua pepeā€¦Pengine utujulishe jinsi ulivyojua kuhusu tovuti hii, au ikiwa sasa umeanza kuwa na uhusiana mpya na Mungu. Ni furaha yetu kujibu swali lolote ambalo unaweza kuwa nalo. Twatarajia kusikia kutoka kwako!