Kuhusu tovuti hii

Tovuti ya StartingwithGod.com ni tovuti ya kukusaidia wewe kukua na kumjua Mungu zaidi. Hakuna uhusiano wowote wenye baraka kubwa ambao mwanadamu anaweza kuwa nao, kushinda kumjua Yesu Kristo kibinafsi.

Tungetaka ujue kwamba . . .

  • Tunaheshimu faragha yako. Sisi hatutakufuata huku na huko katika mtandao eti kwa ajili ya kukufikishia matangazo ya kibiashara, baada ya wewe kutembelea tovuti ya StartingwithGod.com. Unaweza hata kutembelea tovuti yetu mara moja tu, na kutoka hapo usisikie kutoka kwetu tena.

  • Sisi kamwe hatuuzi bidhaa zozote. Pia sisi hatusambazi matangazo ya biashara ya watu wengine.

  • Lakini unaweza kujiandikisha ili upate mfululizo wa maandishi yetu, bila kulipa malipo yoyote yale, na pia bila kuwa na wasiwasi wowote. Sisi hatuwashirikishi (au kuwauzia) watu wengine anwani yako ya barua pepe.

Tovuti ya StartingwithGod.com inakupatia mweke wa kutuuliza swali kwa njia ya kututumia ujumbe wa barua pepe. Nasi tutakufikisha kwenye mtandao wetu wa EveryStudent.com ili uweze kuuliza swali hilo lako. Na tunakuhakikishia kwamba tutakutumia jibu ambalo tumefikiria kwanza (na sio la kutoa tu kwa maandishi mengine na kukutumia), na jibu lenyewe utatumiwa na mtu halisi.

Tovuti ya StartingwithGod.com sasa inapatikana katika lugha zaidi ya 20. Maelfu ya watu kote ulimwenguni wameweza kukua katika uhusiano wao na Mungu kupitia kwa tovuti hii.

Tovuti hii ya StartingwithGod.com ilianzishwa na ingali inaongozwa na mtu mmoja ambaye mbeleni alikuwa kafiri, na ambaye sasa anafanya kazi na shirika la Kikristo lisilo la faida na ambalo linajulikana kama Cru. Kikundi hiki cha Cru ni kikundi kisichoegemea dhehebu lolote na kinafanya kazi kwa kushirikiana na madhehebu mengi ya Kikristo na pia vikundi vya Kikristo kote ulimwenguni. Lengo la Cru ni kusaidia watu wengi kumjua Yesu Kristo kwa njia ya kibinafsi. Kama unataka kujua itikadi za kimsingi za shirika la Cru hebu tutumie barua pepe.

Ni tumaini letu kwamba wewe utaendelea kukua katika uhusiano wako na Mungu na pia katika upendo wake. Hakuna mahusiano mengine ambayo mwanadamu anaweza kuwa nayo ambayo yanaweza kutosheleza shauku zetu za moyoni na mawazo yetu kwa kiwango hiki cha juu kabisa.