Upendo wa Mungu ni Spesheli

Sikiliza makala hii:

Uhusiano na Mungu haufanani na uhusiano mwingine wowote ambao ushawahi kuwa nao. Mungu anakupenda kwa njia spesheli. Upendo wake hauna masharti (hautegemei wewe kutimiza masharti fulani). Mungu anakupenda kwa sababu anakupenda.

“Na Mungui alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake. Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisi tulikuwa tumempenda Mungu kwanza, bali kwamba yeye alitupenda . . .” (1 Yohana 4:9,10).

Yeye hakupendi kulingana na bidii zako. Hakuna jambo lolote ambalo unaweza kutenda ili kumfanya Mungu akupende zaidi ya anavyokupenda sasa—na hakuna jambo ambalo litamfanya Mungu kupunguza upendo wake kwako. Yeye anakupenda hata kuliko unavyojipenda.

Kufikia sasa huenda ikawa mahusiano yako yote ya hapo mbeleni yalikuwa yenye masharti. Upendo kama huu wenye masharti huwa unategemea yale ambalo unafanya. Fanya kazi vizuri kibinafsi au katika timu yako, au ufanye bidii kuwa na mahusiano bora na wenzako, na hapo ndipo “utapendwa.”

Lakini ulipofungua maisha yako kwa Kristo sasa umepata upendo kamili na kukubalika kabisa. Hilo laweza kuwa jambo ngumu wewe kuelewa, hasa ikiwa kwamba hujawahi kujihisi kwamba kuna mtu duniani ambaye anayekupenda na kukubali kabisa. Lakini huo ndio ukweli wa mambo! Walakini, daima wewe hutahisi kwamba Mungu anakupenda. Kuna nyakati zitafika ambapo utatilia shaka sio tu upendo wake Mungu, bali pia kama kwamba Yeye yu hai. Utajihisi kwamba unataka kukata tamaa. Lakini usifanye hivyo.

Mungu alipokupatia maisha haya mapya maisha hayo hayakukufikia yakiwa yamepambwa mapambo mazuri au kunukia manukato bora. Yesu mwenyewe alianza maisha yake duniani katika zizi la ng’ombe ambalo lilikuwa likivunda. Yeye aliishi maisha ya kawaida na hayo ndiyo yatakuwa manukato ya safari yako na Kristo—hakutakuwa na mambo ya kifumba macho, bali utakuwa tu na ahadi ya kwamba Yeye yu nawe maishani mwako.

Mungu anasema, “Nami nimekupenda kwa mapendo ya daima, kwa hiyo nimeendelea kuwa mwaminifu kwako” (Yeremia 31:3).

Kuna mithali moja ya nchi ya Denmark ambayo inasema: “Haja yako kubwa ni kuchukua hatua ya kwenda mbele.” Kujua kwamba Mungu anakupenda ni jambo ambalo litaendelea kukupatia nguvu wakati hatua ya pili itaonekana kuwa ngumu wewe kuchukua: “Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 8:38,39).

Imani yetu hutegemea ukweli ambao Mungu ametujulisha kuhusu nafsi yake. Hasa kwamba Yeye anataka tuamini na kutegemea upendo wake kwetu:

“(Bwana) . . . hupendezwa na watu wamchao, watu wanaotegemea fadhili zake” (Zaburi 147:11).

“Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao, watu ambao wanatumainia fadhili zake” (Zaburi 33:18).

Mfalme Daudi, ambaye Mungu alimsema kwamba yeye ni mtu “anayepatana na moyo wangu” aliamini upendo huo wa Mungu: “Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako; nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako; maana wewe umekuwa ngome yangu na kimbilio langu wakati wa taabu. Ewe uliye nguvu yangu, nitakuimbia sifa; ee Mungu, wewe u ngome yangu; Mungu mwenye kunifadhili!” (Zaburi 59:16,17)

Ili wewe uweze kujua upendo wake Mungu kwa njia kubwa zaidi hebu chukua wiki kadhaa zijazo kusoma Zaburi 103, Yohana 15, na 1 Yohana 4, huku ukitilia maanani jinsi ambavyo upendo wake Mungu umeelezewa katika sehemu hizo za Biblia.